Kiungo Nick Powell ni miongoni mwa wachezaji ambao wataondoka klabuni hapo huku taarifa ya kuondoka kwake ikipokelewa tofauti na mashabiki wa United.
Powell 22, alitabiriwa kuja kuwa mchezaji bora sana alipojiunga na United mwaka 2012, lakini amecheza mechi 3 tu katika kipindi cha miaka 4 kwenye ligi kuu nchini England na sasa Powell anajikuta akitupiwa virago klabuni hapo.
Taarifa za kuchukuliwa kwa mkopo katika klabu za Wigan Athletic, Leicester na Hull City nazo pia zimeonekana kutokuzaa matunda na kuonekana wazi kuwa maisha ya Powell katika soka kuingia matatani.
Hatahivyo mashabiki wa United wamekuwa na maoni tofauti kufuatia kuachiwa kwa Powell katika klabu hiyo,Wengi wakisema kinda huyo hakupewa nafasi ya kuonyesha uwezo wake.
Hizi hapa ni Tweets za mashabiki hao wakieleza hisia zao;
0 comments:
Post a Comment