Sunday, June 12, 2016

HUYU MWINGINE ALIYENASWA NA WEKUNDU WA MSIMBAZI

Simba imemsainisha beki wa Mwadui Emmanuel Semwanza.

Semwanza ameichezea Mwadui kwenye mzunguko wa pili baada ya kununuliwa kwenye kipindi cha usajili wa dirisha dogo akitokea African Lyon, tayari Beki huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuichezea Simba Juzi Alhamisi majira ya saa 5 Usiku.

"Usiku huu tumefanikiwa kumsainisha Semwanza (Emmanuel) kutoka Mwadui ambaye ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwa kwenye orodha yetu. Bado kuna sura nyingine za kazi zinakuja hivyo wapenzi wetu wasiwe na wasiwasi" yalisemwa na kiongozi wa Simba.

Beki huyo nae baada ya kusajiliwa na klabu ya Simba alisema kwa muda mrefu alikuwa na ndoto za kuichezea Simba na hivyo anafuraha kwa kujiunga na wekundu hao wa msimbazi.

"Kwa Muda mrefu nilikuwa na hamu ya kuichezea Simba na nadhani hawajakosea kunisajili. Nataka kuthibitisha uwezo wangu na kuisaidia Simba ifanye vizuri." alisema Semwanza.

Aidha beki huyo aliwashukuru viongozi wa Mwadui kwa ushirikiano waliompa kipindi anaitumikia klabu hiyo na kuwataka watambue kuwa kujiunga kwake Simba ni nafasi kwake kuendeleza kipaji chake katika soka.

0 comments:

Post a Comment