Saturday, February 11, 2017

ligi ya mabingwa Afrika: Yanga waenda Comoro kuikabili Ngaya



Mabingwa wa Tanzania bara kesho watakuwa kibaruani kuiwakilisha Tanzania katika nchi Comoro watakapocheza na mabingwa wa nchi hiyo timu ya Ngaya.

Yanga imeondoka jana ijumaa kuelekea mji wa Moroni nchini Comoro ambapo ndipo mtanange wake utafanyika majira ya 15:00 kwa saa za Afrika Mashariki

Yanga imeondoka na jumla ya watu 30 ikiwemo wachezaji 20 viongozi wa timu 2 na benchi la ufundi lenye watu 8.

Leo jioni itafanya mazoezi katika Uwanja ambao utatumika kesho ili kuuzoe Uwanja na kuwaka viungo sawa kabla ya mchezo.

Wachezaji waliondoka jana ni
 makipa :     Ally Mustafa na Deogratius Munish
Mabeki: Mwinyi Haji, Hassan Ramadhani, Nadir Haroub, Kelvin Yondani, Juma Abdul na Oscar Joshua

Viungo: Deud Kaseke,Haruna Niyonzima,Thaban Kamusoko, Saimon Msuva,Geoffrey Mwashuiya,Saidi Makapu, Juma Mahadhi,Justine Zulu,Kelvin 

Washambuliaji: Yusuph Mhilu,Obrey chirwa, Emmanuel Martin na Amissi Tambwe.

Benchi la ufundi:  George Lwandamina,Noel Mwandila,Edward Samwel Bavu,Juma Pondamali,Juma Zakaria Omary,Hafidhi Saleh Suleiman,Mohamed Omary Mwaliga na Jacob Sospeter Onyango.

Viongozi:  Paul Malume (Yanga Sc) na Mussa Mohamed Kisoki (Tff)

KILALAKHERI WAWAKILISHI WETU KATIKA MICHUANO YA KILAB BINGWA BARANI AFRIKA
Nb:

Mshambuliaji Donald Ngoma atalazimika kuwa nje kwa wiki mbili zaidi ili kuuguza jeraha alilolipata katika mchezo uliopita dhidi ya Stand United, atarejea uwanjani February 25


Michezo mingine kwa siku ya kesho February 12 ni kama ifuatavyo:
Wa All Stars vs Al Ahli Tripoli 17:00

Gambia Ports Authority vs Sewe  17:00

Leopards de Dolisie vs UMS de Loum 17:30

Cotonsport vs  Atlabara 17:30

Barrack Young Controllers vs Stade Malien Bamako 19:00


Sony de Ela Nguema vs Al Merrikh 19:30

0 comments:

Post a Comment