Wednesday, June 1, 2016

HAWA NDO WATAKAOAMUA MECHI KATI YA STARS NA MISRI

Waamuzi wanne kutoka Gabon, ndio watakochezesha mchezo wa kimataifa kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Mapharao wa Misri utakaofanyika Jumamosi Juni 4, 2016 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.




Mchezo huo utakaoanza saa 10.00 jioni ni wa kutafuta nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) zitakazofanyika Gabon ambako mwamuzi wa kati atakuwa ni Meye Bastrel atakayesaidiwa na Mihundou Ganther na Vinga Theophile wakati Mwamuzi wa akiba (mezani) atakuwa Otogo Eric.

Wakati waamuzi wote wanatoka Gabon, Kamishna wa mchezo huo ni Tarig Atta Salih kutoka Sudan.

Maandalizi ya mchezo huo yamekamilika kwa Shirikisho Soka la Tanzania (TFF) kuipokea timu ya taifa ya Misri inayotarajiwa kuingia kesho Juni mosi, 2016 ambako wataweka kambi kambi kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempiski, Dar es Salaam.

Taifa Stars imeweka kambi Hoteli Urban Rose ambayo pia iko katikati ya jiji la Dar es Salaam tangu iliporejea kutoka Kenya jana Mei 30,2016 ambako ilicheza timu ya Taifa ya Kenya maarufu kama Harambee Stars. Katika mchezo huo uliofanyika Jumapili Mei 29, mwaka huu timu hizo zilitoka sare ya 1-1.

CHANZO: TFF

Related Posts:

  • TAIFA STARS KUCHEZA NA HARAMBEE STARS Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa na timu ya Taifa Kenya (Harambee Stars) Mei 29, 2016 jijini Nairobi. Mche… Read More
  • Yanga Yatinga Fainali Kombe La Shirikisho Coastal Union imepoteza mechi ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Yanga baada ya washabiki wake kuwa chanzo cha Mwamuzi kuvunja mchezo huo uliofanyika Aprili 24, 2016 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga. Uam… Read More
  • Kikosi Cha Yanga Leo Dhidi Ya Coastal Union NUSU FAINALI  KOMBE LA SHIRIKISHO (FA CUP). Coastal Union SC Vs Young African SC. Uwanja- Mkwakwani KIKOSI CHA YANGA LEO. Deogratius Bonaventura Munish Juma Abdul Japhary Oscar Fanuel Joshua Nadir Haroub Canna… Read More
  • Farid Mussa Aanza Majaribio La Liga WINGA machachari wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Farid Mussa, ameanza majaribio rasmi nchini Hispania akiwa na kikosi cha timu ya CD Tenerife inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini humo. Farid,… Read More
  • Yanga Kufanya Uchaguzi Tarehe Hii Hapa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo imetangaza Juni 05, 2016 kuwa siku ya Uchaguzi Mkuu wa viongozi ndani ya klabu ya Young Africans SC ya jijini Dar es salaam. Akiongea na waandishi … Read More

0 comments:

Post a Comment