Sunday, May 8, 2016

MASHABIKI WAMPA MKONO WA KWAHERI NYOTA HUYU ANAEJIUNGA NA LIVERPOOL



Mchezaji wa kimataifa wa Cameroon Matip (24) ameichezea klabu ya Schalke 04 katika maisha yake yote ya soka hadi sasa, amecheza michezo 260 katika klabu katika mashindano yote tangu aanze kucheza klabuni hapo mwaka 2009.

Kabla ya mechi yao waliyocheza katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Augsburg, mashabiki wa Schalke 04 walitandaza bango kubwa nyuma ya lango moja la goli likiwa na ujumbe uliotafsiriwa kuwa “Kwa miaka 16 umejitolea kila kitu chako kwa ajili ya Schalke-Asante sana Jimmy”

Matip amefunga magoli 3 katika ligi msimu huu. Ni mchezaji kipenzi cha mashabiki wa Schalke na itakuwa vigumu kuziba pengo lake kwani amekuwa na kiwango kizuri sana katika mechi zote za ligi alizocheza.

Mwisho wa Msimu huu Matip anatarajia kujiunga na Klabu ya Liverpool, ikiwa tayari ameshasaini makubaliano ya awali na klabu hiyo ya Liverpool.

Related Posts:

  • TFF YAJA JUU SUALA LA KESSYShirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) limesema litaingilia kati suala la mchezaji Ramadhan Kessy aliyesajiliwa na Yanga huku Simba wakikataa kuiandikia barua Yanga kumruhusu mchezaji huyo kuanza kuitumikia klabu hiyo. … Read More
  • TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATANO JUNI 22,2016Tetesi Za Usajili Barani Ulaya  Bale Kupewa Mkataba Mrefu Madrid Mchezaji wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale anatarajiwa kupewa mkataba mpya utakaomuweka Santiago Bernabeu Kwa zaidi ya miaka 6. Barcelona Yamuwinda Ga… Read More
  • KIPA AONDOKA CHELSEA KWA MKOPAMlinda Mlando wa Chelsea Mitchell Beeney ameondoka klabu hapo kwa mkopo na kujiunga na klabu inayoshiriki ligi daraja la kwanza ya Crawley. Beeney 20, hajawahi kucheza mechi yoyote ya ligi kuu tangu ajiunge na Chelsea na m… Read More
  • KIMESHAELEWEKA YANGA WAPYA WOTE RUKSA ISIPOKUWA HUYUWachezaji wote wapya wa Yanga wamethibitishwa kuwa huru kuanza kuitumikia klabu hiyo isipokuwa Hassan Ramadhan Kessy. Yanga imewasajili wachezaji watano hadi sasa ambao ni Andrew Vicent, Juma Mahadhi, Ben Kakolanya, Hassan… Read More
  • JAMIE VARDY AONGEZA MKATABA LEICESTER CITYMfungaji bora wa ligi kuu nchini Uingereza Jamie Vardy ameongeza mkataba wa miaka minne katika klabu yake ya Leicester city. Mshambuliaji huyo hivi karibuni alihusishwa na kujiunga na klabu ya Arsenal lakini uvumi huo sasa… Read More

0 comments:

Post a Comment