Yanga imewasajili wachezaji watano hadi sasa ambao ni Andrew Vicent, Juma Mahadhi, Ben Kakolanya, Hassan Ramadhan pamoja na Obrey Chilwa. Katika wachezaji hao ni Hassan Ramadhan tu ambaye bado taratibu zake za uhamisho hazijakamilika baada ya Simba kukataa kuwaandikia barua Yanga kumruhusu mchezaji huyo kuanza kuitumikia Yanga.
Hata hivyo klabu ya Yanga imewaandikia barua Simba SC kuwauliza kama kuna pingamizi lolote juu ya mchezaji huyo huku wakiambatanisha na mkataba wa Kessy unaoonyesha kumalizika Juni 15 na kwamba endapo Simba hawatojibu barua hiyo basi watachukua hatua ya kulipeleka suala hilo TFF ili waweze kulitolea maamuzi.
0 comments:
Post a Comment