Kwa mara ya kwanza idadi ya mashabiki waliohudhuria uwanjani katika mechi za La Liga imezidi watu milioni 14.
Taasisi inayoshughulika na ligi kuu nchini Hispania La Liga imekusanya takwimu kutoka katika mechi 848 zilizochezwa kwenye ligi kuu (Primera Division) na Ligi Daraja la kwanza (Segunda Division) na kisha kupata idadi hiyo ya mashabiki.
Idadi ya tiketi 14,010,099 ziliuzwa katika kipindi cha msimu wa 2014/2015 huku idadi ya mashabiki ikiwa ni 13,792,333.
Hii ni rekodi ambayo haijawahi kufikiwa na ligi nyingine yoyote.
0 comments:
Post a Comment