Wednesday, June 22, 2016

TETESI ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO JUMATANO JUNI 22,2016

Tetesi Za Usajili Barani Ulaya

 Bale Kupewa Mkataba Mrefu Madrid
Mchezaji wa kimataifa wa Wales, Gareth Bale anatarajiwa kupewa mkataba mpya utakaomuweka Santiago Bernabeu Kwa zaidi ya miaka 6.

Barcelona Yamuwinda Gabriel Jesus
Jesus 19, anawindwa na mabingwa wa La Liga, Barcelona na Mabingwa hao wamekuwa wakimfuatilia kwa karibu katika mechi zake anazocheza kwenye klabu yake ya Palmeiras.


Rasmi: Morata Asaini Real Madrid
Morata 23, amekuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na mabingwa hao wa Uefa Champions League mara 11 akitokea Jeventus kwa uhamisho wa paundi milioni 32.


Lukaku Hana Haraka Ya Kuondoka Everton
Wakala wa Mshambuliaji huyo amesema Chelsea watakumbana na changamoto nzito katika harakati zao za kutaka kunasa saini ya Lukaku, kwani bado anahitaji kubaki Everton.

Leicester City Kumsainisha Hernandez
Hernandez atajiunga na Leicester City kwa mkataba wa miaka wa minne kwa mujibu wa mabingwa hao wa ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2015/16

Redknapp Asema West Ham Haitamuuza Payet
Wagonga nyundo hao wameweka kiwango cha paundi milioni 60 kwa klabu itakayohitaji kumsajili Payet, Hata hivyo Redknapp amesema hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo anayefanya vizuri katika michuano ya Euro inayoendelea huko nchini Ufaransa.

Related Posts:

  • PICHA ALIYOPOST MKEWE MOURINHO YAZUA UTATA UJIO WA POGBA MAN U Mashabiki wa Manchester United wamekuwa katika hali ya sintofahamu kuhusu ujio wa Pogba Man U hasa baada ya Mke wa Jose Mourinho kupost picha ambayo Mourinho amemjumuisha Pogba katika hesabu zake. Picha hiyo ilipostiwa k… Read More
  • PAUL POGBA AWAAGA MARAFIKI ZAKE JUVENTUS Licha ya kiwango kidogo alichoonyesha katika michuano ya Euro 2016 katika ardhi ya nyumbani, Paul Pogba anabaki akihusishwa sana na kujiunga na klabu ya Manchester United chini ya kocha Mourinho. Manchester United wanao… Read More
  • YANGA WAMWONGEZEA MKATABA PLUIJM Mabingwa wa ligi kuu Vodacom na wawakilishi pekee Afrika Mashariki katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF CC), Yanga wamemwongezea mkatabawa miaka miwili kocha wao Hans Van Pluijm. Kocha huyo ambaye ame… Read More
  • RASMI: PAUL NONGA AONDOKA YANGA Aliyekuwa mchezaji wa Yanga Paul Nonga ameondoka klabuni hapo na kujiunga na klabu ya Mwadui baada ya muda mrefu kuuomba uongozi wa klabu hiyo imuuze kwenye klabu ambayo atapata nafasi ya kucheza. Paul Nonga akisaini mkata… Read More
  • TAARIFA YA WAKALA WA PAUL POGBA YAZUA GUMZO Uhamisho wa Paul Pogba kwenda Manchester United umezidi kuchukua sura mpya baada ya sasa hivi kuonekana dili hilo bado kabisa kukamilika. Wakala wa Pogba, Minola Raiola, ametumia akaunti yake ya twiter kukanusa uvumi una… Read More

0 comments:

Post a Comment