Sunday, May 8, 2016

INTER MILANI YAFUZU KUSHIRIKI EUROPA LEAGUE 2016/17


Inter Milan imetinga katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi kuu nchini Italia, Serie A, baada ya ushindi wa 2 – 1 walioupata dhidi ya Empoli. Vijana hao wa Roberto Mancini walishindwa kufuzu nafasi ya kucheza UEFA Champions League baada ya kukubali kipigo cha magoli 2 – 0 dhidi ya Lazio wikiendi iliyopita lakini ushindi wao dhidi ya Empoli  jana umewafanya wajihakikishie nafasi yao ya kushiriki michuano ya UEFA EUROPA League Msimu Ujao. Magoli ya Inter yalifungwa na Icard dakika ya 12 na Perisic 40 na lile la Empoli lilifungwa na Pucciarelli dakika ya 37.

0 comments:

Post a Comment