Sunday, May 8, 2016

KIMENUKA EMIRATES, WENGER, SANCHEZ VITANI




Hali imekuwa sio ya kawaida kati ya Alex Sanchez na manager wake Arsenal Wenger, Sanchez alitolewa katika mchezo dhidi ya Norwich zikiwa zimebaki dakika sita mchezo kumalizika, kitendo hicho hakikumfurahisha Sanchez na alivyotoka  hakutaka hata kupeana mkono na Wenger na akaenda moja kwa moja katika vyumba vya kubadilishia nguo, ikionekana wazi kuwa alichukizwa na kitendo cha kutolewa katika mchezo huo.

Imeripotiwa kuwa Sanchez ataihama klabu hiyo mara baada ya mkataba wake kumaliza hapo 2018.

Sanchez ameonekana kutokuwa na msimu mzuri kutokana na kiwango chake kuonekana kimeshuka, lakini kocha Wenger amekanusha uvumi kwamba hana maelewano mazuri na mchezaji huyo kufuatia kitendo alichokifanya Sanchez, huku akisema kitendo cha Sanchez kuonyesha kuchukia baada ya kutolewa uwanjani ni kuonyesha kwamba alikuwa anatamani aendelee kucheza na sio kwamba kuna tofauti baina yao.


Lakini habari za ndani ya klabu hiyo zinaonyesha Wenger hafurahishwi na kiwango na mchezaji huyo kwa sasa. Arsenal wanacheza na Manchester City leo na licha ya hali inavyoendelea klabuni hapo baina ya Wenger na Sanchez, mchezaji huyo anategemewa kucheza katika mechi hiyo.

0 comments:

Post a Comment