Sunday, May 8, 2016

HABARI 5 KUBWA ZA USAJILI ULAYA LEO MAY 8,2016


Rodgers Kurudi Swansea
Imeripotiwa kwamba Rodgers aliyekatimuliwa na Liverpool amekubali kurudi katika Klabu yake ya zamani ya Swansea kwa Mshahara wa Paundi 90,000/- sawa na zaidi ya Sh. Milioni 284 kwa wiki.

Szczesny Aishauri Chelsea Kuhusu Nainggolan
Mlinda mlango wa zamani wa Arsenal Szczesny anayecheza katika klabu ya Roma kwa sasa ameishauri Chelsea kumnunua Mbelgiji mwenzake Nainggolan, huku ikiripotiwa kuwa Szczesny ndio muunganishaji mkubwa wa hiyo dili.

Wenger Akiri Kumuhitaji Kante
Kocha Mfaransa Arsene Wenger anaamini midfielder wa Leicester City amekuwa ni miongoni mwa wachezaji walioonyesha kiwango cha hali ya juu zaidi katika ligi msimu huu, na anahakika kwamba licha ya wao kumuhitaji, vitajitokeza vilabu vingi kuonyesha nia ya kumnasa mchezaji huyo.

Sturridge Asema Hana Tatizo Na Klopp
Mshambuliaji wa klabu ya Liverpool Daniel Sturridge ametupilia mbali uvumi unaomuhusisha yeye na hatima yake katika klabu ya Liverpool, akisisitiza kwamba anafurahia maisha katika klabu hiyo huku akisema kwamba hakuna ufa kati yake na Klopp. Sturridge anahusishwa na kujiunga na klabu ya Arsenal, baada ya Wenger kuonyesha kutaka kuinasa saini ya mchezaji huyo.

Ben Arfa Katika Mazungumzo Na Barcelona

Nyota huyo mwenye miaka 29 amekuwa ni moja kati ya wachezaji walioonyesha kiwango bora zaidi katika Ligi kuu Ufaransa maarufu kama Ligue 1, huku Mkataba wake na klabu yake ukiwa unaisha mwishoni mwa msimu huu, Barcelona wameonyesha nia ya kutaka  kumsajili nyota huyo.

0 comments:

Post a Comment