Friday, June 17, 2016

KOCHA MWENYE REKODI ZA KIMATAIFA KUTUA SIMBA

Harakati za usajili katika klabu ya Simba bado zinaendelea na habari za hivi karibuni zinasema makocha wanne kutoka katika nchi nne tofauti wamejitokeza kutaka kuinoa klabu hiyo.

Geofrey Nyange "Kaburu" (Makamu mwenyekiti wa klabu ya Simba) amesema kuwa kitu cha kwanza wanachokusudia kukifanya ni kuleta kocha mzungu mwenye rekodi ya kimataifa ambaye atawasaidia katika kuchagua wachezaji wa kuwasajili watakaoimarisha kikosi hicho.
Kaburu alisema hawezi kutaja nchi wanazotoka makocha hao, kikubwa ni kuwa wamevutiwa na ubora wa wasifu wao na ufahamu wao mzuri wa soka la Afrika hasa ukanda wa Afrika mashariki.

"Bado tunaendelea na mchakato wa kusaka kocha, tayari tuna maombi kutoka kwa makocha wa nchi nane tofauti, wapo wawili ambao tumevutiwa nao na tunatarajia kufanya nao mazungumzo ili kuona yupi tumchukue" alisema kaburu.

"Shida yetu kubwa ni kuiona Simba ikifanya vizuri kwenye ligi na kumaliza uteja wa kufungwa na Yanga kama ilivyokuwa msimu uliopita, ndiyo maana tukaamua kutafuta kocha mwenye kulijua vizuri soka la Afrika Mashariki na wachezaji wenyewe na tunafurahi mazungumzo yanaenda vizuri" aliongeza Kaburu.

Simba walishafanya mazungumzo na kocha Mzimbabwe Kalisto Pasuwa lakini  mipango ilionekana kushindikana na kumkosa kocha huyo.

0 comments:

Post a Comment