Pia, ameeleza masikitiko yake ya kuumia na kushindwa kuisaidia timu yake kufikisha malengo ya kutwaa mataji na kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu uliopita.
Akihojiwa na tovuti ya Azam FC Kapombe alisema: “Nilijisikia vibaya kutokana na mimi kuwa mmojawapo wa wachezaji waliojiwekea malengo ya kuifikisha mbali Azam FC pale ilipotarajiwa na watu wengi, kama vile kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu, Kombe la FA na kufika robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika. “Lakini siwezi kulaumu sana kwa sababu ni kitu ambacho kilitokea mbeleni, ila nimeumia zaidi kwa kuwa sikuweza kufikisha malengo ya msimu kwa namna tulivyojipangia,” alisema.
Kapombe pia aliushukuru uongozi wa Azam FC kwa kumjali kwa kipindi chote alichokuwa akitoa mchango wake kwenye timu hiyo na hata alipopata matatizo na kudai kuwa amefarijika sana kwa hilo.
“Ninachowaahidi viongozi na mashabiki nitaendelea kupigania timu kwa moyo mmoja na kuongeza juhudi zaidi ili kuifanya Azam FC ifike mbali zaidi,” alisema.
Beki huyo wa zamani wa Simba na AS Cannes ya Ufaransa, aliwaomba mashabiki, wachezaji wenzake pamoja na uongozi wamuombee kwa Mungu ili aweze kurejea tena dimbani msimu ujao.
“Kwa mashabiki, wachezaji wenzangu na viongozi nawaomba tu tuzidi kuombeana kheri, ili niweze kurudi vizuri na niweze kuimarika zaidi kiafya ili nifanikiwe kujiunga na wenzangu kwa maandalizi ya msimu ujao na kuifikisha timu katika malengo yale ambayo viongozi wamepanga,” alisema.
Licha ya kukosa sehemu kubwa ya mechi za mwisho za msimu uliopita, Kapombe alifanikiwa kuwa beki pekee wa Ligi Kuu Tanzania Bara aliyefunga mabao mengi zaidi kwenye ligi akifunga manane.
0 comments:
Post a Comment