Saturday, June 18, 2016

KIUNGO MPYA SIMBA TISHIO KWA MKUDE, NDEMLA

Simba imefanikiwa kumsajili Kiungo Mzamiru Yasini akitokea katika klabu ya Mtibwa Sugar.

Yasini amesema hayupo tayari kukaa benchi hivyo atahakikisha anapambana na wakongwe ili kujihakikishia nafasi yake katika kikosi cha kwanza.
Kiungo huyo amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu hiyo ya Simba.

Mzamiru amesema anafahamu changamoto anayoenda kukutana nayo kwenye timu hiyo na tayari ameanza kujipanga kwa kufanya mazoezi ya nguvu ili kumshawishi kocha aweze kumjumuisha kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo.

"Naenda Simba nikifahamu nafasi yangu ina wachezaji wengi wazuri na wana uzoefu, lakini nimejipanga kumshawishi kocha aweze kunitumia kwenye kikosi cha kwanza kwa sababu nisingependa kukaa benchi." alisema Yasini.

Aidha Kiungo huyo aliongeza kuwa anafahamu ukubwa wa klabu ya Simba, klabu ambayo mashabiki wake wanahitaji ushindi kila siku, hivyo kuahidi kujituma na kushirikiana vizuri na wenzake ili kurudisha mataji ambayo yamekuwa adimu katika klabu hiyo.
Yasini pia aliwaomba mashabiki kumpa sapoti ili aweze kutumia vizuri ujuzi wake kwa ajili ya kuwapa raha mashabiki hao.

Bonyeza hapa ku-Like Page ya Soka24 Facebook

Related Posts:

  • CHIRWA ATUA JANGWANI KWA SH. MILIONI 240Mshambuliaji raia wa Zambia, Obrey Chirwa amejiunga na Yanga kwa dau la sh. Milioni 240 akitokea katika klabu ya FC Platinum za Zimbabwe. Chirwa ameifungia Platinum mabao matano katika mechi nane alizocheza kwenye ligi kuu… Read More
  • KIFAA KIPYA YANGA KUTUA LEO JANGWANIWalter Musona Mshambuliaji kutoka FC Platinum ya Zimbabwe anatarajiw kuwasili Daresalaam leo alasiri kwa ajili ya mazungumzo na klabu ya Yanga. Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka katika klabu ya Yanga, tayari mambo yo… Read More
  • HUYU NDO KOCHA MPYA BRAZILTite ametajwa kuwa kocha mpya wa Brazil baada ya Dunga kutupiwa virago kufuatia matokeo mabovu waliyoyapata Brazil Copa America 2016. Tite Tite 55, anachukua nfasi ya Dunga aliyetimuliwa mara baada ya Brazil kutolewa hatu… Read More
  • KOCHA MWENYE REKODI ZA KIMATAIFA KUTUA SIMBAHarakati za usajili katika klabu ya Simba bado zinaendelea na habari za hivi karibuni zinasema makocha wanne kutoka katika nchi nne tofauti wamejitokeza kutaka kuinoa klabu hiyo. Geofrey Nyange "Kaburu" (Makamu mwenyekiti … Read More
  • RUVU SHOOTING KUKIPA NGUVU KIKOSI CHAORuvu Shooting ipo katika mipango ya kusajili wachezaji saba ili kujiimarisha kabla hawajaanza kipute cha ligi kuu Vodacom msimu wa 2016/17. kwa sasa Ruvu Shooting inaendelea na kambi kwenye uwanja wa Mabatini Mlandizi, Pwa… Read More

0 comments:

Post a Comment