Friday, May 27, 2016

"SITOICHEZEA TENA SIMBA MSIMU UJAO" MAJABVI

Kiungo wa Kimataifa wa Simba Jastice Majabvi, ameweka wazi kuwa hatoichezea tena timu hiyo msimu ujao baada ya mkataba wake kuwa umemalizika.



Kiungo huyo amesema mipango yake kwa sasa ni kueleka nchini Sweden kujaribu bahati yake na ataachana na vijana wa Msimbazi. Maamuzi hayo ya Majabvi yanakuja baada ya Mke wake kuajiriwa nchini Sweden hivyo amesema anataka kwenda kumpa kampani.

"Nawashukuru viongozi wa Simba pamoja na mashabiki wa timu hiyo kwa ushirikiano mzuri walionipa siwezi kuendelea kucheza soka kwa sababu nataka kuwa karibu na familia yangu ambayo imepata uhamisho nchini Sweden" alisema Majabvi.

0 comments:

Post a Comment