Home »
Usajili
» HABARI KUBWA ZA USAJILI BARANI ULAYA LEO IJUMAA MEI 27, 2016
Ibrahimovic Apewa Ofa Nono Na Klabu Ya China
Straika huyo anonekana kuvutiwa na Man U kwa klabu za ligi kuu ya Uingereza lakini huenda akashawishika na ofa kubwa aliyopewa na klabu ya china endapo atakubali kwenda kucheza soka huko.
Joe Allen Hajaamua Hatima Yake Liverpool
Midifielda wa Liverpool amekuwa akihusishwa na kuondoka klabuni hapo huku yeye mwenyewe akisema hatafanya mazungumzo yoyote na klabu hiyo hadi aiwakilishe Wales katika michuano ya Euro itakayofanyika mapema mwezi Juni huko Ufaransa.
West Ham Yakata Tamaa Kwa Lacazette
Straika wa Lyon anakubalika hata na uongozi wa juu wa klabu hiyo lakini kuna uwezekano akaondoka klabuni hapo huku West Ham wakionekana kukata tamaa ya kumnasa Straika huyo.
Liverpool Yajiunga Mbio Za Kumwania Mane
Mario Gotze hajawahakikishia Liverpool kujiunga na klabu hiyo na hivyo kuwafanya Liverpool kugeuzia mawindo yao kwa supastaa wa Southampton Mane, ambaye pia anatakiwa na klabu zingine za ligi kuu nchini Uingereza.
Skrtel Kuondoka Liverpool
Beki wa kimataifa wa Kati raia wa nchini Slovakia Skrtel alijiunga na mwaka 2008 akitokea Zenit na sasa ameonyeshwa mlango wa kutokea klabuni hapo, huku klabu ya Uturuki ya Besiktas ikiwa tayari imeonyesha nia ya kumsajili beki huyo.
0 comments:
Post a Comment