Mayanga amepanga kumsajili mlinda mlango Hussein Sharifu kwa ajili ya kuziba pengo la Beno Kakolanya aliyetimkia Yanga. Sharifu amekosa nafasi ya kucheza katika kikosi cha kwanza cha kocha Mecky Maxime tangu aliporejea timu hiyo akitokea Simba na kumuacha Said Mohamed akitamba kwenye nafasi hiyo karibu msimu mzima wa ligi kuu Tanzania.
Kocha huyo amesema kuwa anafahamu vizuri uwezo wa Sharifu na ndiyo maana anataka kumchukua uli wakafanye naye kazi huku akiamini kuwa ataziba vizuri pengo hilo lililoachwa na Kakolanya.
"Najua siwezi kupata ushindani kwa sababu nina mahusiano mazuri na uongozi wa Mtibwa Sugar, naamini hawawezi kuninyima kipa huyo ambaye kwangu naamini atanisaidia kwenye msimu ujao" alisema Mayanga.
Aidha Mayanga amesema licha ya kukaa benchi mlinda mlango huyo, kwa kipindi atakachokuwa nae yeye atahakikisha anamnoa na kumrudisha katika kiwango chake kilichokamfanya asajiliwe na Simba pamoja na kuitwa na timu ya taifa "Taifa Stars"
0 comments:
Post a Comment