Friday, June 24, 2016

SIMBA YAPEWA SOMO

Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Rage ameutaka uongozi wa Simba uliopo madarakani kuacha malumbano na wachezaji.

Kumekuwa na kutokuelewana kwa siku za hivi karibuni baina ya wachezaji na viongozi wa Simba kitu ambacho kwa kiasi fulani kimechangia matokeo mabaya ya klabu hiyo. Rage amesema viongozi wanatakiwa kupunguza malumbano na wachezaji ili kujenga kikosi imara ambacho kitarudisha heshima ya timu hiyo kwa kufanya vizuri katika michuano mabalimbali.

Mwenyekiti huyo alisema matokeo mabaya ya Simba yamechangiwa na viongozi wa klabu hiyo kuwafukuza wachezaji wazuri bila sababu za msingi jambo ambalo.

"Niseme ukweli kwamba Yanga ndiyo timu bora hivi sasa hapa kwetu Tanzania kwa sababu wamesajili wachezaji wazuri wenye uwezo na wamekaa pamoja kwa muda mrefu tofauti na Simba yetu ambayo kila msimu tunakuwa tukisajili waachezaji wapya ambao wamekuwa wakihitaji muda kuzoeana na wengine wamekuwa wakifukuzwa pasipo sababu za msingi" alisema Rage.

Rage pia alisema kitu kingine ambacho kimekuwa kikiwatatiza Simba ni uongozi wa klabu hiyo kuogopa vikao vya wanachama ambavyo kwa asilimia kubwa vinakuwa na nia njema.

"Mimi nawashauri wenzangu kutanguliza busara mbele na wasiogope vikao vya wanachama pia nawatakia mafanikio mema kuelekea mkutano mkuu utakaofanyika Julai 10. mwaka huu cha msingi wajitahidi kufanya usajili mzuri msimu huu kwa kutumia pesa za usajili wa Emmanuel Okwi na Mbwana Samatta ili kurudisha mafanikio ya Simba" alimalizia Rage.

Bonyeza Hapa Ku-Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook

0 comments:

Post a Comment