Friday, June 24, 2016

HII NDIO KUFURU WALIYOIFANYA YANGA KWA MZAMBIA

Yanga imemsajili kiungo mshambuliaji Obrey chirwa raia wa Zambia akitokea klabu ya FC Platinum ya nchini Zimbabwe.

Hizi ndio pesa atakazozivuna mchezaji huyo katika klabu ya Yanga.

Obrey atakusanya jumla ya Dola 168,000 ambazo ni sawa na (Sh. milioni 363.476) ikiwa ni mshahara wake kwa kipindi cha mkataba wake wa miaka miwili.
Chirwa pia atakuwa anakusanya dola 7,000 ambazo ni sawa na Sh. milioni 15.14 kwa mwezi, mshahara ambao umekuwa ni habari ya mjini huko nchini Zimbabwe kwa sasa.
Kama hiyo haitoshi, Uhamisho wake kutoka katika klabu ya Platinum kutua Yanga, umewagharimu Yanga kiasi cha dola laki moja (100,000) sawa na Sh. milioni 216.3, pesa ambazo ziligawanywa na yeye kupata kiasi cha dola 30,000 sawa na sh. milioni 64.9 pesa ya kusaini Jangwani wakati dola 70,000 (shi.milioni 151.449) ikichukuliwa na klabu yake ya zamani ya FC Platinum.

Licha ya hizo fedha zote, Yanga pia imempangia nyumba yenye vyumba viwili mchezaji huyo ili aishi na familia yake.

Kwa ujumla pesa ambazo Chirwa atazikusanya katika klabu ya Yanga zinaweza kutumika kulipa mishahara ya wachezaji 11 kwenye timu za wachezaji wa bei poa.

Kwa mujibu wa Msemaji wa klabu ya FC Platinum, Chizo Chizondo, usajili huo wa Chirwa umevunja rekodi katika kipindi hiki na kuwafanya nyota wengine nchini humo kutaka kucheza ligi kuu ya Tanzania.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

0 comments:

Post a Comment