Yanga iliwaandikia Simba barua kutaka kujua kama kuna pingamizi lolote juu ya mchezaji huyo baada ya kukataa kutoa kiasi cha fedha ambacho Simba walikihitaji, Yanga pia ilipeleka nakala ya barua hiyo TFF ili endapo Simba watashindwa kulitolea maamuzi hilo mapema ili TFF ichukue hatua.
Hali hiyo imewafanya Simba kupanga kukutana lengo likiwa ni kujadili masuala mbalimbali likiwemo na Suala la Kessy.
Mkuu wa Kitengo cha mawasiliano Simba, Haji Manara amesema uongozi wake haujajibu barua hiyo mpaka pale watakapokutana.
"Leo (Jana) baada ya kumaliza kufuturu tunakutana kwa ajiili ya kupanga vitu mbalimbali lakini suala la barua waliotuandikia Yanga pia itajulikana hapo" alisema Manara.
Aidha Manara alisema baada ya kikao hicho atazungumza na waandishi wa habari leo ili kuwajulisha kilichoamuliwa kwenye kikao hicho.
"Siwezi kusema chochote mpaka kikao kitakapomalizika na baada ya hapo kutakuwa na mkutano na waandishi wa habari leo hivyo tusubiri" aliongeza Manara.
Yanga walishindwa kumtumia kessy katika mchezo wao wa kwanza waliocheza Algeria kutokana na kutopata ruhusa kutoka kwa klabu ya Simba, na iwapo Simba wataweka pingamizi kuhusu mchezaji huyo watatakiwa kuwa na hoja za msingi za pingamizi hilo ambalo litasikilizwa na kamati ya Sheria na hadhi ya wachezaji ya TFF.
0 comments:
Post a Comment