Baada ya msimu mbaya uongozi wa klabu ya Simba umeahidi kuachana na wachezaji kutoka katika nchi jirani za Kenya na Uganda na kupanga kuelekeza macho yao Afrika Magharibi.
Ofisa habari wa klabu ya Simba Hajji Manara akizungumza na Goal amesema, wameamua kufikia maamuzi hayo baada ya kutofurahishwa na tabia za wachezaji hao huku akikiri kwamba wamechangia kwa kiasi kikubwa timu kufanya vibaya hasa katika mechi za mwisho za msimu wa ligi kuu Vodacom.
"Tumeshindwa kutimiza malengo yetu msimu huu kwasababu wachezaji wa kigeni hasa kutoka mataifa ya Kenya na Uganda, wameshindwa kutupa kile tulichotrajia kutoka kwao na tumepanga kuachana nao ili kutafuta wengine kutoka mataifa ya Magharibi" alisema Manara.
Simba imemaliza katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi kuu Vodacom msimu wa 2015/16
0 comments:
Post a Comment