Friday, May 27, 2016

CHRISTIANO RONALDO HATAKI KUSIKIA MWANAE ANAITAJA BARCELONA

Christiano Ronaldo amezungumza kuhusu familia yake huku akiweka bayana kuwa mapenzi yake makubwa na Madrid hayawezi kuruhusu kumwacha kijana wake akiishabikia Barcelona.



"Kijana wangu amebadilisha maisha yangau katika mambo mengi sana" alisema Ronaldo alipohojiwa na Jugones mtangazaji wa kituo cha televisheni cha La Sexta cha Nchini Hispania.

"Haiwezekani kumwacha anaisapoti Barcelona kwa sababu ni damu yangu, ila kama aking
ang'ania hilo basi nitamwachia"

"Mama Yangu ndio nguzo ya familia na ananisaidi sana kumtunza kijana wangu, hana mama, ila ana baba na mama kwa wakati mmoja ambaye ni mimi"

Akizungumzia sakata la Mourinho na Man United Ronaldo alisema anaamini litakuwa jambo zuri sana kama Man U wakimpa kazi Mourinho.

"Natumaini ya kuwa Mourinho atayarudisha yale makali ya United, na ataifikisha timu mbali"

Ronaldo anatarajiwa kuiwakilisha klabu yake kesho katika mchezo wa fainali kombe la klabu bingwa Ulaya dhidi ya Atletico Madrid.

0 comments:

Post a Comment