Klabu ya Pelileo Sporting Club ya nchini Ecuador imeishushia kipigo klabu ya Indi Native cha magoli 44 - 1 katika mchezo wa ligi daraja la tatu nchini humo.
katika mchezo huo mshambuliaji wa timu ya Pelileo, Ronny Medina alifunga magoli 18. Baada ya kichapo hicho Rais wa timu ya Indi Native, Diego Culequi alisema kichapo hicho hakukitarajia huku akisema wachezaji wake hawakuzoeaa hali ya joto kali ambalo yeye anaamini lilichangia timu yake kupokea kichapo hicho.
Huko nchini Scotland rekodi ya timu kufunga magoli mengi katika mchezo mmoja ilikuwa inashikiliwa na Arbroath FC ya Scotland iliyofunga mabao 36 - 0 dhidi ya Bon Accord miaka 131 iliyopitwa.
Mwaka 2002, Mechi ya Ligi kuu Nchini Madagascar ilitoa kali ya mwaka baada ya mabingwa wateule AS Adema kuwafunga watani wao wa Jadi Stade Olympique I'Emyrne magoli 149 - 0. Idadi hiyo ilifika baada ya wachezaji wa Olympique kuwa wanajifunga kwa makusudi baada kukasirishwa na maamuzi ya mwamauzi wa mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment