Friday, July 22, 2016

TAARIFA YA WAKALA WA PAUL POGBA YAZUA GUMZO

Uhamisho wa Paul Pogba kwenda Manchester United umezidi kuchukua sura mpya baada ya sasa hivi kuonekana dili hilo bado kabisa kukamilika.

Wakala wa Pogba, Minola Raiola, ametumia akaunti yake ya twiter kukanusa uvumi unaoenea kwa kasi hivi sasa kuwa Nyota huo wa Ufaransa ameshafikia makubaliano na klabu ya Manchester United baada ya kuandika kwenye ukurasa wake wa twiter kuwa hakuna dili lolote lililokamilika kuhusu Pogba bali ni bla bla nyingi tu zilizoenea hivi sasa.

Siku ya Jumatano zilitoka taarifa kuwa uhamisho wa karne unaomuhusisha Pogba kujiunga na Man U tayari umeshakamilika na kwamba linasubiriwa tangazo maalumu tu kutoka kwa  klabu hiyo.

Hatahivyo mawakala wa wachezaji hupenda kukanusha taarifa hata zile zinazokuwa na ukweli ndani yake ili mradi lengo lao wanalokusudia litimie, kitu ambacho kauli hiyo ya wakala wa Pogba huenda ikawa ni miongoni wa tabia tu za mawakala wa soka katika kupunguza uvumi fulani.

Mashabiki wa Manchester United ambao tayari walishakuwa wameziamini na kuzipokea kwa shangwe taarifa za kukamilika kwa uhamisho wa Pogba kutoka Juve na kujiunga na klabu yao, wamenyong'onyeshwa na kauli hiyo ya Raiola kwamba hakuna chochote kilichokamilika hadi hivi sasa.
Ungana Na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA  Kwa Habari Za Haraka Za Soka Kote Ulimwenguni.

0 comments:

Post a Comment