Wednesday, August 31, 2016

Arsenal Yakamilisha Usajili Wa Shkodran Mustafi

Klabu ya Arsenal imetangaza rasmi kumsajili beki wa kati wa Valencia Shkodran Mustafi kwa ada ya uhamisho ambayo haijawekwa wazi.

Licha ya thamani ya uhamisho wa mchezaji huyo kutowekwa wazi lakini habari za chini chini zinasema mchezaji huyo ameigharimu Arsenal kiasi cha pauni milioni 41.

Alipohojiwa baada ya kukamilisha usajili huo kocha wa klabu ya Arsenal, Arsene Wenger alisema Mustafi ni mchezaji mzuri, yupo katika umri sahihi pia utakaomuwezesha kucheza soka kwa muda mrefu.

“Yupo katika umri sahihi. Ana uzoefu mkubwa,” Wenger aliiambia tovuti ya Arsenal. “Ni mchezaji ambaye anajua nini anapaswa kufanya na kwa wakati gani anayejua kuchezea mpira pia.”

“Tumepata mchezaji mzuri sana lakini mwenye matarajio ya muda mrefu.”

Awali Mustafi aliwahi kuichezea klabu ya Everton japo hakupata nafasi sana ya kucheza na hii inakuwa mara ya pili kwa mchezaji huyo kucheza ligi kuu nchini Uingereza.
===============
Stori Kubwa Zinazotikisa Anga La Michezo Hivi Sasa;

Rasmi:Wilfred Bony Atua Stoke City

"Yanga Timu Bora Zaidi Tanzania" Pluijm

Omog Ashusha Presha Za Wana Msimbazi


Aubameyang Aitamani Real Madrid


Simba Yabadili Gia Angani


Ungana na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA

Related Posts:

  • ARSENE WENGER KUSAINI MKATABA MWINGINE NA ARSENAL Uongozi wa klabu ya Arsenal umepanga kumwongeza mkataba wa miaka 2 kocha wake Arsene Wenger mkataba ambao anatarajiwa kusaini October mwaka huu, lengo likiwa ni kupata muda wa kutosha wa kumtafuta atakaekuwa mrithi wa We… Read More
  • HIZI NDO BLA BLA ZA MOURINHO NA MAN U TANGU 2015 Jose Mourinho amekuwa akihusishwa na kujiunga na United tangu Disemba 2015. Jose Mourinho amekuwa akihusishwa na kuchukua mikoba ya Van Gaal United tangu atimuliwe na Chelsea. Soka24 inakuletea mtiririko wa matukio ya… Read More
  • KIBARUA CHA ROBERTO MARTINEZ CHAOTA NYASI Akiwa ameshinda mechi moja tu kati ya 10 walizocheza hivi karibuni, huku wakiruhusu kipigo cha goli 3-0 kutoka kwa Sunderland Jumatano iliyopita, hitaji la wapenzi wa Goodison Park kuona kocha huyo anatimuliwa lilizidi … Read More
  • MAURICIO POCHETTINO AONGEZA MKATABA SPURS Kocha wa klabu ya Tottenham Spurs Mauricio Pochettino amesaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaomuweka klabuni hapo hadi mwaka 2021. Pochettino alishatangaza wiki 2 nyuma kuwa alishafanya mazungumzo ya awali na klabu hiy… Read More
  • HATIMA YA VAN GAAL MAN UNITED YAWEKWA WAZI Louis Van Gaal amehakikishiwa na mabosi wa United kuwa ataendelea kubaki katika klabu hiyo hadi mwisho wa mkataba wake kwa mujibu wa ripoti ya Daily Star. Mdachi huyo anayeinoa United amekuwa akisemwa sana juu ya uwezo … Read More

0 comments:

Post a Comment