Akiwa ameshinda mechi moja tu kati ya 10 walizocheza hivi karibuni, huku wakiruhusu kipigo cha goli 3-0 kutoka kwa Sunderland Jumatano iliyopita, hitaji la wapenzi wa Goodison Park kuona kocha huyo anatimuliwa lilizidi kuwa kubwa.
Roberto Martinez hakuonekana katika mazoezi na timu hiyo Alhamisi hii asubuhi, huku Everton wakisubiriwa kutoa tamko rasmi kuhusu kocha huyo. Vyombo vikubwa vya habari vikiwemo BBC Sports na Sky Sports vimesharipoti kuondoka kwa Martinez klabuni hapo kabla Everton wenyewe hawajatoa tamko rasmi.
Everton wanashika nafasi ya 12 katika msimamo wa ligi kuu nchini Uingereza huku kukionekana uwezekano mkubwa wa timu hiyo kushuka zaidi ya hapo ilipo hadi kufikia nafasi ya 16 endapo matokeo ya mchezo wao wa mwisho katika ligi yatakuwa mabaya.
0 comments:
Post a Comment