Thursday, May 12, 2016

FAINALI UEFA CHAMPIONS LEAGUE KUAMUA HATIMA YA RONALDO MADRID


Superstaa wa Real Madrid Christiano Ronaldo amekubali kubaki Real Madrid kwa Sharti moja tu. Ronaldo amesema yupo tayari kubaki Santiago Bernabeu ikiwa tu Real Madrid watafanikiwa kuifunga Atletico Madrid katika mchezo wao wa fainali ya UEFA Champions utakaopigwa Milan May 28.

Kama Madrid watafungwa katika fainali hiyo basi Ronaldo ataondoka klabuni hapo huku klabu anayopenda kwenda kucheza ikiwa ni Manchester United klabu yake ya zamani, Wakala wa Christiano Ronaldo Jorge Mendes amekubaliana na Real Madrid kuhusu mkataba mpya wa Christiano Ronaldo utakaomuweka Madrid hadi mwaka 2020 kwa mshahara wa Paundi milioni 15.8 kwa mwaka.

Lakini Ronaldo amesema hatima yake na klabu hiyo ya Madrid inategemea mchezo wao wa fainali dhidi ya Atletico Madrid utakaochezwa uwanja wa San Siro mwishoni mwa mwezi huu.

Paris Saint-Germain wameonesha nia kubwa ya kutaka kumsajili Ronaldo wakiwa wameshaandaa paundi milioni 63.3 za uhamisho lakini Ronaldo anaonyesha kutokufurahishwa na mazingira ya ligi kuu nchini Ufaransa maarufu kama Ligue 1.

Kama Man United wakiwa na cash hakutakuwa na kikwazo tena kwa Mreno huyo kutua Man U.

0 comments:

Post a Comment