Sandro Ramirez (20), alikuwa akitabiriwa kuwa ni shujaa ajae wa Barcelona. Akiwa ametokea katika Academy ya klabu hiyo ya Barcelona, lakini ameambiwa na kocha wake Luis Enrique kuwa hana mipango nae.
Kwahiyo Barcelona wamemuweka Sandro sokoni kwa klabu itakayomuhitaji iweze kumsajili na kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo, Sandro yupo sokoni kwa dau la paundi milioni 7.8.
Tottenham walionyesha nia ya kumtaka straika huyo mapema mwaka huu lakini walimkosa kutokana na kufungwa kwa dirisha la usajili kabla Sandro ajasaini na Tottenham, lakini bado wanatumaini la kumnasa mchezaji huyo kutoka Barcelona katika msimu ujao wa usajili.
0 comments:
Post a Comment