Louis Van Gaal amehakikishiwa na mabosi wa United kuwa ataendelea kubaki katika klabu hiyo hadi mwisho wa mkataba wake kwa mujibu wa ripoti ya Daily Star.
Mdachi huyo anayeinoa United amekuwa akisemwa sana juu ya uwezo wake kufuatia matokeo mabaya ya klabu hiyo na hasa baada ya kutolewa mapema katika michuano ya UEFA Champions League.
Van Gaal bado ana mwaka mmoja umebaki katika mkataba wake lakini Jose Mourinho amekuwa akimnyima usingizi Gaal kutokana na kuhusishwa mara kwa mara na kujiunga na klabu hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya Daily Star, Mabosi wa United wamemuhakikishia Van Gaal kuendelea kuitumikia klabu hiyo hadi utakapomalizika mkataba wake.
“Niko hapa na napambana” alinukuliwa Van Gaal
“Licha ya lawama zote ninazotupiwa na vyombo vya habari, lawama nzito kutoka kwa wakongwe wa soka, na zingine kutoka kwa watu wa aina mbalimbali mimi naamini katika uwezo wangu, naamini katika uwezo wa Manchester na naamini pia katika wachezaji wangu” aliongeza Van Gaal.
Manchester United wana nafasi ya kuvaa medali za dhahabu endapo tu watafanikiwa kuifunga Crystal Palace katika fainali ya FA Cup itakayopigwa Wembley May 21.
0 comments:
Post a Comment