Sunday, May 15, 2016

ACACIA KUSITISHA UDHAMINI NA STAND UNITED


KAMPUNI ya ACACIA inayoidhamini timu ya Stand United ya mkoani Shinyanga imesema itaondoa udhamini wake na klabu ya Stand kama Stand itaendeshwa kama kampuni. Taarifa hizo zimekuja mara baada ya Stand kutangaza kuwa kwa sasa itaendeshwa kama kampuni tofauti na ilivyokuwa awali.Baada ya taarifa hizo kuifikia kampuni hiyo ya ACACIA, uongozi wa kampuni umeiandikia uongozi wa klabu ya Stand United barua inayowataarifu Stand juu ya ACACIA kutaka kusitisha udhamini wao na klabu hiyo kama Stand itaendeshwa kama kampuni.

Mwenyekiti wa Stand United Amani Vicent amethibitisha kupokea barua hiyo kutoka katika kampuni ya ACACIA huku akikiri kuwa ni kweli kwamba Stand kwa sasa itaendeshwa kama kampuni huku akidai kuwa uongozi wa Stand utakaa na Mabosi wa ACACIA ili kuweka mambo sawa lengo likiwa ni kuwaomba wasisitishe udhamini wao licha ya ukweli kuwa Stand ni kampuni na itabaki kuwa hivyo.

Itakumbukwa kuwa kampuni ya ACACIA iliingia udhamini na klabu ya Stand United mara baada ya kumalizika kwa msimu wa ligi wa mwaka 2014/15, udhamini wenye thamani ya  shilingi bilioni 2.4 kwa muda wa miaka miwili.

0 comments:

Post a Comment