MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Dar Young Africans Amis Tambwe, amemaliza mchezo wa jana dhidi ya Ndanda FC bila ya kufunga goli, Tambwe anayeongoza katika orodha ya wafungaji bora katika ligi kuu Tanzania bara msimu huu wa 2015/16 ameshafunga magoli 21.
Akizungumza jana baada ya mechi yao na Ndanda FC iliyoisha kwa sare ya 2 - 2 Tambwe alisema siku zote yeye anapenda kuwa juu ya wengine na ndio maana anapambana sana ili kutimiza azima yake hiyo katika kila mchezo anaopata nafasi ya kucheza, akizungumzia mchezo huo Tambwe alisema amepambana kwa uwezo wake ila hajafanikiwa kupata goli, huku akimwombea mabaya mpinzani wake Hamisi Kiiza anayemnyemelea kwa karibu katika chati hiyo ya ufungaji akiwa ameshafunga magoli 19. Tambwe aliongeza kwa kusema anaomba kwa mungu Kiiza asifunge goli lolote katika michezo yote miwili iliyobaki ili yeye afanikiwe kutwaa kiatu cha dhahabu msimu huu.
"Nataka asifunge goli lolote katika mechi zao zilizobaki, adui yako lazima umuombee mabaya" yalikuwa maneno ya Tambwe alipozungumza baada ya mechi jana katika uwanja wa taifa.
Yanga wamebakiwa na mechi moja wakati Simba wao wakiwa na mechi mbili, hivyo kumfanya Tambwe kuwa na wasiwasi na Kiiza kwamba huenda akaongeza idadi yake ya magoli katika mechi 2 zilizobaki na kumpiku katika tuzo ya mfungaji bora wa msimu ambapo mshindi huondoka na kitita cha zaidi ya shilingi milioni 5 za kitanzania.
0 comments:
Post a Comment