Sunday, May 15, 2016

VITA YA KUWANIA NAFASI YA PILI VPL KUENDELEA TENA LEO


LIGI kuu Tanzania bara inatarajia kuendelea tena leo katika viwanja viwili. Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa watawakaribisha vijana wa Msimbazi Simba SC wakati huko Tanga Azam FC itachuana na African Sports.
Simba wanashika nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi wakiwa wamejikusanyia pointi 59 katika michezo 28 waliyocheza, wakati Azam FC wao wapo katika nafasi ya 2 kwa jumla ya pointi 63 walizozipata katika michezo 28 waliyocheza.

Timu hizi zitashuka viwanjani leo zote zikiwa na dhamira ya kupata ushindi ili kuweza kuzipata milioni 40 anazopewa mshindi wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom Premier League, endapo Azam FC watashinda mchezo wa leo basi moja kwa moja watakuwa washindi wa pili kwa kuibwaga Simba SC kwani watakuwa wamefikisha pointi 66 huku wakibakiwa na mchezo mmoja, wakati huo Simba wao wakishinda mechi ya leo watafikisha pointi 62 na kubakiwa na mchezo mmoja ambao hata wakishinda watafikisha pointi 65 wakiachwa kwa pointi 1 na Azam FC.

Hali hii ndo inazifanya mechi za leo kuwa ni za kuvutia licha ya kuwa bingwa tayari alishapatikana na kukabidhiwa kombe lake. Azam FC watakuwa wanapambana kupata ushindi katika mchezo wake leo, Simba nao watapigana vikali kuhakikisha wanashinda huku wakiwaombea wapinzani wao Azam FC kupoteza katika mchezo wao dhidi ya African Sports.


0 comments:

Post a Comment