Timu ya soka ya Simba imezidi kupoteza matumaini ya kunyakua ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara baada ya kukubali kichapo cha Goli 1 - 0 toka kwa Toto Africans ya Mwanza.Katika mchezo huo ambao wadau wengi wa soka waliipa Simba nafasi ya ushindi, kibao kiligeuka na kujikuta wakizidiwa kila idara na mapema katika dakika ya 20 mchezaji Wazir Junior alifanikiwa kupachika goli safi na laushindi kwa timu yake ya Toto Africans.
Mpaka mpira unakwisha Toto Africans walikuwa wanaongoza kwa goli 1 dhidi ya Simba
0 comments:
Post a Comment