Sunday, April 17, 2016

Hapatoshi Leo Tena Taifa


Patashika za ligi kuu ya kandanda tanzania bara zinaendelea tena leo kwa mchezo mmoja tu kupigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es salaam ukiwakutanisha wenyeji Simba SC dhidi ya Toto Africans ‘wana kishamapanda’kutoka jijini Mwanza.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwa pande zote,ambapo Simba inataka kurejea kwenye kiti chake cha enzi kileleni kwa kufikisha pointi 60 huku Toto Africans wakitaka kujinyanyua kuukwepa mstari wa kuporomoka daraja kutoka katika nafasi ya 11 iliyopo sasa.

Simba kwa sasa inashikilia nafasi ya pili ikiwa na pointi 57 nyuma ya Yanga wenye pointi 59 huku Azam FC wakishikilia nafasi ya tatu kwa kuwa na pointi 55.

Kwa mujibu wa kocha wa Saimba,Jackson Mayanja,amesema vijana wake wapo tayari kukusanya pointi zote zilizobakia ili kumaliza wa kwanza na hatimae kushiriki michuano ya klabu bingwa barani afrika msimu ujao.

0 comments:

Post a Comment