Bondia Ibrahim Class
|
Bondia mtanzania Ibrahim Class ‘King Class Mawe’ameendelea kutamba katika mapigano yake nje ya nchi baada ya usiku wa kuamkia jana kufanikiwa kumtwanga Mjerumani huko Panama City Amerika Kusini.
Pigano hilo la raundi 8 na lisilo la ubingwa,lilikuwa kivutio kwa watazamani kwani kila bondia alikuwa akirusha makonde mazito lakini mtanzania alifanikiwa kumzidi mpinzani wake na hatimaye kuibuka mshindi kwa pointi na kujipatia umaarufu kwa mapromota walijojitokeza kushuhudia pigano hilo.
Hili ni pambano la pili kwa Ibrahim Class kushinda nje ya nchi likitanguliwa na lile dhidi ya Mzambia na kufanikiwa kuunyakua mkanda wa WPBF Afrika,na kuzidi kulitangaza taifa lake nje ya mipaka.
0 comments:
Post a Comment