Sunday, April 17, 2016

Samatta Habari Nyingine Jamani

Samatta akishangilia Baada ya kufunga bao

Nahodha wa Tanzania, Mbwana Samatta ameendelea kung’ara Ulaya baada ya kuifungia tena klabu yake, KRC Genk katika ushindi wa 2-1 ugenini dhidi ya wenyeji SV Zulte-Waregem.

Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya Ubelgiji uliofanyika Uwanja wa Regenboogstadion mjini Waregem, Samatta alifunga bao la kwanza dakika ya saba tu kwa kichwa akimalizia krosi ya mkongwe wa umri wa miaka 25, Mbelgiji Thomas Buffel.
Beki wa Kongo mzaliwa wa Ufaransa, Marvin Baudry akajifunga katika harakati za kuokoa dakika ya 15 kuipatia Genk bao la pili, kabla ya mshambuliaji Msenegali, M'Baye Leye kuifungia SV Zulte-Waregem bao la kufutia machozi kwa penalti dakika ya mwisho ya kipindi cha kwanza.

Goli hilo linakuwa la nne kwa Samatta katika mechi tisa alizocheza tangu ajiunge na Genk Januari mwaka huu akitokea TP Mazembe ya DRC.

Mabao mengine alifunga katika ushindi wa 4-0 na 4-1 dhidi ya KV Oostende na 3-2 dhidi ya Club Brugge.

0 comments:

Post a Comment