Mshambuliaji huyo ambae hivi karibuni aliuandika uongozi wa Yanga barua akiwa anaomba umuuze kwenye timu nyingine kutokana na kuchoshwa na benchi, sasa amezitaka klabu zinazomhitaji zifanye mazungumzo na Yanga ili kufanikisha uhamisho wake.
Nonga hajajumuishwa katika kikosi cha Yanga kilichoenda kucheza na MO Bejaia, Algeria hivyo amesema tupo tayari hata kwa kupunguza kiasi cha mshahara ilimradi tu yeye aondoke Yanga.
"Nitafurahi kama kuna timu yoyote itajitokeza kipindi hiki tuweze kufanya biashara, nipo tayari kupunguza mshahara wangu ili timu iweze kuninunua na kuichezea msimu ujao, na najua viongozi wa Yanga ni waungwana hawatokataa ofa itakayofika mezani kwao." alisema Nonga.
Nonga alijiunga na Yanga akitokea Stand United, tangu ajiunge na Mabingwa hao wa Ligi kuu na kombe la shirikisho hajapata muda mwingi wa kucheza na hivyo kuona kila dalili za kiwango chake kupotea kwani mchezo wa soka unahitaji kucheza mara kwa mara ili uwe fiti na ujiamini unapokuwa dimbani.
Hali ya kukaa benchi imemfanya Nonga kusema yupo tayari hata kutolewa kwa mkopo kwani anachokitaka yeye ni kucheza.
0 comments:
Post a Comment