Kiwango chake kiliwavutia viongozi wa Tenerife na kuona haja ya kuwa na winga huyo hivyo kinachosubiriwa sasa ni kukamilika kwa mazungumzo yanayoendelea baina ya klabu hizo mbili juu ya Farid ili aweze kwenda kuanza maisha mapya katika ligi daraja la kwanza nchinni Hispania.
Farid mwenyewe amesema anaamini kwenda kwake Hispania kutasaidia kukuza kiwango chake tofauti na akibaki Tanzania.
"Ninatamani hata leo uongozi wangu unipe ruhusa kwa sababu mazingira niliyoyaona kule nilipokuwa kwenye majaribio yamenipa hamasa ya kucheza na kuamini kiwango changu kitapanda zaidi ya hapa, lakini pia kwenda kwangu Hispania kutafungua milango kwa wachezaji wengine wa kitanzania kuaminiwa na kusajiliwa huko." alisema Farid.
Safari ya Farid nchini Hispania itasaidia kuamsha hamasa kwa wachezaji wetu wa Kitanzania wanaoamini kucheza Yanga na Simba ndo mwisho wa mafanikio yao ya soka na kuwafanya waangalie mbele zaidi kwani hilo pia litasaidia kuitanganza Tanzania kimataifa na kuwa na idadi kubwa ya watanzania wanaocheza Ulaya na hatimaye kupata kikosi bora cha taifa.
Farid atakuwa Mtanzania wa pili kucheza Ulaya baada ya Mbwana Samatta anayeitumikia klabu ya KR Genk ya nchini Ubelgiji.
0 comments:
Post a Comment