Sunday, June 19, 2016

KIWANGO KIBOVU CHA HAJI MWINYI CHAMUUMIZA PLUIJM

Kiwango cha beki wa kushoto wa Yanga Haji Mwinyi kinaonekana kushuka hali inayomfanya kocha Hans Pluijm kutafuta namna ya kulifanyia kazi suala hilo.

Haji Mwinyi ni beki mwenye kipaji kikubwa anayeweza kuimudu vizuri nafasi yake uwanjani, lakini siku za hivi karibuni kiwango chake kinaonekana kushuka kwa kasi kitu kinacholeta maswali mengi miongoni mwa mashabiki wa soka.
Hali hiyo imepelekea hata kocha Pluijm kumtumia mara kwa mara Oscar Joshua kwenye nafasi hiyo.

Mwinyi pia alivurunda katika mechi dhidi ya Misri, katika mchezo huo Mwinyi Haji ndiye alisababisha magoli yote mawili kitu kilichopelekea kocha Mkwasa kumtoa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mohamed Hussein "Zimbwe Jr".

"tumekaa naye chini na kuzungumza naye kumpa ushauri. Nina imani atarejea kwenye kiwango chake cha kawaida. kwani kichwa chake kimetulia na kiko tayari kusikiliza ushauri." alisema Kocha Pluijm.

"kila kitu kinahitaji muda na nina imani atarejea kwenye ubora wake haraka sana, anafanyia kazi tunayomwambia na anajituma mazoezini." aliongeza kocha huyo.

Andrew Vicent "Dante" aliyesajiliwa na Yanga hivi karibuni anamudu kucheza nafasi hiyo na kusajiliwa kwake kunaweza kusaidia kulipunguza tatizo la nafasi hiyo katika kikosi hicho.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

0 comments:

Post a Comment