Home »
Kitaifa
,
Usajili
» SIMBA WAMNASA MSHAMBULIAJI HATARI ZAIDI, AAHIDI GOLI KILA MECHI ASIPOFUNGA AKATWE MILIONI
Timu ya Simba Sports club imekuwa katika wakati mgumu kwa takribani misimu minne sasa, hali hiyo pia imepelekea viongozi wa klabu hiyo kutokuwa na amani kwa kile kinachoondelea katika timu yao.
Zacharia Hanspope amesema safari hii watafanya vizuri katika usajili ili kukiimarisha vizuri kikosi chao kiweze kuleta ushindani mkubwa katika mashindano yajao. Kauli hiyo inakuja baada ya Hanspoppe kusema kwamba kuna straika mmoja hatari sana ambaye ametaka kujiunga na Simba aitoe Simba ilipo na kuirudisha pale ilipokuwa,
kwa mujibu wa Hanspoppe Straika huyo amesema endapo atasajiliwa na Simba na asipofunga goli lolote katika kila mechi basi akatwe kiasi kikubwa cha fedha kutoka katika mshahara wake, kitu ambacho kimempa imani Zacharia na kuahidi kuvunja benki ili kumnasa mchezaji huyo.
Akizungumza na gazeti la Mwanaspoti Hanspoppe ameweka bayana kuwa kamati yao ya usajili imeamua kufanya kweli na kushusha wachezaji hatari zaidi katika kikosi chao.
"Mfano Mzuri ni Mshambuliaji mmoja ambaye nafanya naye mazungumzo, ameniambia wazi kwamba anataka mshahara wa dola 2500 lakini akatuambia kama atamaliza mechi yoyote bila kufunga bao yuko tayari akatwe dola 500 (shilingi milioni 1) katika mshahara wake huo, mtu wa namna hii anaonyesha wazi anajiamini na kazi yake" alisema Hanspoppe alipohojiwa na gazeti la Mwanaspoti.
Hanspoppe hakutaka kutaja jina la mchezaji huyo ila amesema wao wapo tayari kumsajili kwani ameonyesha nia ya kufanya kazi na Simba.
0 comments:
Post a Comment