Thursday, May 26, 2016

SALAMU ZILIZOTUMWA NA YANGA KWA WAPINZANI WAO BAADA YA KUITANDIKA AZAM FC 3 - 1 ZIMEFIKA, TP MAZEMBE IMEJIBU HIVI

TIMU ya Yanga jana imefanikiwa kutwaa taji la pili msimu huu kombe la shirikisho TFF baada ya kuitwanga Azam FC 3 - 1 na tayari wapinzani wao katika kombe la shirikisho barani Afrika TP Mazembe wameonyesha kukubali kiwango cha Yanga.


Yanga imepangwa Group A na Timu za TP Mazembe, Medeama na MO Bejaia, kiwango cha Yanga msimu huu kimezidi kukua kwa hali ya juu kitu kinacholeta hofu kwa timu pinzani pindi zinapokutana na Yanga. TP Mazembe  itacheza na Yanga June 28 mwaka huu. Mazembe inaamini kuwa ni kweli Yanga kwa sasa imekuwa na kiwango bora, kiwango ambacho hata wao wanaamini watakumbana na upinzani mkali pale watakapokutana.

Katika tovuti yao TP Mazembe wamesema kuwa Yanga imerejesha kujiamini kwake hasa baada ya mechi yao na Al Ahly iliyochezwa Misri. Lakini Mazembe wamesema licha ya kasi hiyo ya Yanga kwa sasa, watakapokutana nao itakuwa ngumu kwa Yanga na kwamba Thomas Ulimwengu atawathibitishia Yanga kuwa Mazembe ni bora zaidi.

"Yanga has stored the confidence among Pharaohs. It will be daunting, do not doubt, Thomas ULIMWENGU will confirm it to you" hayo ni maneno ya TP mazembe katika tovuti yao.


Mchezo wa mpira wa miguu hauna tofauti na michezo mingine yote duniani hasa pale linapokuja suala la kutambiana, Mazembe wameyasema haya katika kuwaweka Yanga tumbo joto lakini kwa siku za hivi karibuni TP Mazembe haijawa katika ubora wao huku wataalamu wa soka wakisema kuondoka kwa Samatta Klabuni hapo kumechangia hali wanayopitia Mazembe kwa sasa.

0 comments:

Post a Comment