Thursday, May 26, 2016

MAMBO MATATU YANAYOMPA HOFU KOCHA PLUIJM ENDAPO MANJI ATAPIGWA CHINI YANGA

Yanga imekuwa na mafanikio makubwa katika kipindi hiki ambacho ipo chini ya uongozi wa Yusuf Manji, na Uchaguzi wa Yanga uko karibuni kufanyika. Tayari kocha wa timu hiyo Hans Van Pluijm ameonyesha wasiwasi wake kama ikitokea Manji akaachia madaraka au kupigwa chini klabuni hapo.


Gharama za timuRipoti zinasema kuwa timu ya Yanga inatumia zaidi ya Sh. Milioni 95 katika mechi 2 za kimataifa ambazo Yanga inacheza dhidi ya timu moja, fedha hizo zikiwa zinalipwa na Manji, hivyo kuondoka kwake kunampa Hans hofu kubwa.

Mishahara Minono Inayolipwa kwa Wachezaji Na Viongozi wa Benchi la Ufundi na Makocha.Hakuna ubishi kuwa kikosi cha Yanga kwa sasa ni miongoni mwa vikosi bora zaidi Afrika Mashariki na hii inatokana na kazi Nzuri ya Manji kwa kuwalipa vizuri wachezaji, viongozi wa Benchi la Ufundi pamoja na makocha kiujumla. Hivi juzi viongozi wa Simba walisikika wakisema kilichowafanya wachelewe kuwalipa wachezaji mishahara yao kwa wakati ni kuchelewa kwa fedha hizo kutoka kwa wadhamini wao, lakini kwa upande wa Yanga Manji anatoa pesa zake pale za wadhamini zinapochelewa ili tu kuweka hali ya utulivu klabuni hapo.Pia huduma nzuri ambazo Yanga inazipata chini ya Uongozi wa wake.

UsajiliTimu ya Yanga kwa sasa imejumuisha wachezaji mbalimbali kutoka katika sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi, Kocha Hans anamsajili mchezaji yoyote anayemtaka kutokana na ushirikiano mzuri anaoupata kutoka kwa bosi wake. Wachezaji wanaboreshewa mikataba yao kitu kinachowafanya wajitume na kuipenda kazi yao hali inayolenda matokeo chanya kwa wanajangwani.

Licha ya hofu zote hizo anazokumbana nazo Hans, uchaguzi wa Yanga ndo utakaoamua nani atashika hatamu katika klabu hiyo.

0 comments:

Post a Comment