Thursday, May 26, 2016

TFF YAKATAA KUWA MWENYEJI KOMBE LA KAGAME

Shirikisho a Soka Tanzana (TFF), limetangaza kutoandaa michuano ya kuwania Kombe la timu za nchi wanachama wa Shirikisho la Soka la Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), maarufu kama Kombe la Kagame kwa mwaka 2016 kama ilivyopendekezwa.



Sababu za TFF ya kutoandaa fainali hizo ni kwa kubanwa na ratiba ya michuano ya kitaifa na kimataifa.

Awali mkutano mkuu wa CECAFA, uliamua Zanzibar iwe mwenyeji wa michuano ya Kagame.Baadaye kwa sababu zilizo nje ya uwezo wa ilionekana Zanzibar hawataweza kufanya.

Baada ya hapo TFF ilianza kuangalia uwezekano wa mashindano haya kwa kumshirikisha mabingwa wa 2015/16 ambao ni Yanga.

Kutokana na ratiba ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAFCC) iliyotolewa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF), kipindi ch Juni hadi Agosti, 2016 Yanga watakuwa na kwenye michuano ya CAF hatua ya makundi hivyo ushiriki wao CECAFA utakuwa mgumu ilihali michuano ya CECAFA imepangwa kufanyika Juni na Julai, mwaka huu.



CHANZO: TFF

0 comments:

Post a Comment