Thursday, July 21, 2016

SIMBA WAIPANIA NDANDA FC

Katibu mkuu wa Simba, Patrick kahemela ameapa kurudisha furaha na kuachana na machungu ya kutoka vichwa chini katika mechi zao za ligi kuu.

Kiongozi huyo amesema Ndanda FC ndiyo itakuwa ya mfano kwani imepania kuwapa raha mashabiki katika mchezo huo.
Ligi kuu Vodacom inaanza kutimua vumbi Agosti 20 mwaka huu ambao klabu ya Simba itaanza kwa kumenyana na Ndanda FC katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

"Ukweli kama uongozi tumepania kufanya mabadiliko makubwa na kuirudisha timu kwenye ubora wake, tunachotaka ni kuona mashabiki wa Simba kuanzia msimu ujao wanatoka viwanjani wakiwa wenye furaha na siyo huzuni kama ilivyokuwa huko nyuma na ndiyo maana tumekuwa tukipambana kuleta wachezaji wengi wakigeni ili kujenga timu imara yenye ushindani."

Simba haikufanya vizuri kwenye msimu uliopita, Katibu huyo aliongeza kuwa anajua ushindani uliopo kati yao na Yanga lakini hilo ni jambo zuri kwao kwa sababu itakuwa sifa kubwa wao kubeba taji la ligi kuu kwa kushinda timu zenye uimara.

“Tupo makini kusema kweli kwa sababu tusingependa msimu ujao kuona tunaendelea kuwapa wakati mgumu mashabiki wetu na wapenzi wa Simba kama ilivyokuwa huko nyuma tunataka msimu ujao uwe wa vicheko na furaha mwanzo hadi mwisho bila kuihofia timu yoyote,” alisema Kahemele.

Kwa sasa Simba wapo Morogoro wakipiga kambi kujiandaa na ligi kuu msimu ujao. Na hivi juzi wamewaleta wachezaji wengine wawili wa kigeni ambao ni Masoud Cedrick kutoka DR Congo pamoja na Sanga Bahende.
Ungana Na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA  Kwa Habari Za Haraka Za Soka Kote Ulimwenguni.

0 comments:

Post a Comment