Thursday, July 21, 2016

YANGA WAMWONGEZEA MKATABA PLUIJM

Mabingwa wa ligi kuu Vodacom na wawakilishi pekee Afrika Mashariki katika michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika (CAF CC), Yanga wamemwongezea mkatabawa miaka miwili kocha wao Hans Van Pluijm.

Kocha huyo ambaye ameipa mafanikio makubwa klabu ya Yanga ikiwemo kufikisha katika hatua ya makundi kombe la shirikisho barani Afrika alisema anaipenda sana klabu ya Yanga na kwamba anajitahidi kila uchao kuhakikisha analeta heshima na furaha kwa viongozi, wanachama na mashabiki wa klabu hiyo.

“Naipenda hii klabu sikuzote nimekuwa nikifanya kazi kwa kutanguliza heshima na mapenzi ambayo watu wa Yanga wamekuwa wakinionyesha, sasa nimeongeza mkataba ambao hata familia yangu ina furaha na hilo,” amesema Pluijm

Aidha Pluijm aliongeza kuwa anachangamoto kubwa sana katika kuhakikisha Yanga inaendelea kufanya vizuri zaidi ya walipofikia mwaka huu huku akiweka wazi kuwa anajua ni kazi ngumu lakini atapambana ili kufikia malengo.

“Changamoto yangu kubwa sasa ni kuhakikisha Yanga inafanya mazuri zaidi kuzidi ya haya tuliyoyapata msimu huu najua haitakuwa kazi rahisi lakini hakuna namna lazima tupambane kila mmoja na nafasi yake kuweza kufikia malengo.”
Ungana Na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA  Kwa Habari Za Haraka Za Soka Kote Ulimwenguni.

0 comments:

Post a Comment