Thursday, July 21, 2016

HII NDO SABABU YA YANGA KUTOKUUZA WACHEZAJI ULAYA

Kocha mkuu wa Yanga, Hans van Pluijm amesema wachezaji wengi wa Tanzania hawako tayari kucheza mpira wa kulipwa ulaya.

Kwa muda mrefu imeonekana kuwa Yanga inawabania sana wachezaji wake hasa pale wanapopata nafasi ya kutakiwa na klabu mbalimbali nje ya nchi ukilinganisha na mahasimu wao klabu ya Simba, akitolea maelezao suala hilo koch Pluijm amesema utayari wa wachezaji wenyewe ndio unasababisha hali hiyo.

“Kwanza sijui kuhusu kutakiwa kwa wachezaji wangu kwenye nchi za Ulaya. Pili kila mmoja anapaswa kujiuliza kama wako tayari kwa ajili ya soka la kulipwa. Wote tunapenda kuona wachezaji wetu wakifanikiwa,” alisema Pluijm.

Pluijm aliongeza kuwa kama kuna kitu cha kubadilisha kwenye soka la Tanzania ni basi ni mtazamo wa wachezaji na viongozi kuelekea kwenye soka la kulipwa.

“Kwa baadhi ya wachezaji ni kama utamaduni wa kushangaza kubadili akili na mtazamo wao. Lakini kama unataka kubadili kitu fulani kwa ujumla kwenye soka la Tanzania basi ni mtazamo wao kuelekea kwenye soka la kulipwa... “Kubadili mtazamo wao na kuwafanya wawe na shauku ya kutaka kupata tuzo binafsi, kwa klabu zao na timu ya taifa,” alisema Pluijm.

Kocha huyo aliwataka wachezaji wa Yanga kuiga Mfano wa Samatta ambaye kwa sasa anacheza katika klabu ya KRC Genk ya nchini ubelgiji.
Ungana Na Soka24 Facebook, Bonyeza  HAPA  Kwa Habari Za Haraka Za Soka Kote Ulimwenguni.

Related Posts:

  • MIPANGO YA JULIO KATIKA USAJILIKocha wa Mwadui FC, Jamhuri Kiwelu "Julio" amesema yeye hana mpango wa kusajili wachezaji wa kigeni katika kikosi chake. Julio amesema lengo lake ni kutoa fursa kwa wachezaji wa ndani waweze kuonyesha uwezo wao ili waje ku… Read More
  • KIPAUMBELE NAMBA 1 CHA SIMBA KATIKA USAJILI HIKI Simba ipo katika harakati za kuimarisha kikosi chao kwa kuhakikisha hawafanyi makosa katika usajili kipindi hiki ambacho dirisha la usajili limefunguliwa. Uongozi wa Simba umesema kipaumbele chao cha kwanza katika kipindi … Read More
  • BOCCO ATAJA KILICHOWAPONZA AZAM FCNahodha wa timu ya Azam FC, John Bocco amesema kuwa kushindwa kupata mafanikio katika msimu uliopita kumechangiwa na kuwakosa wachezaji wao muhimu katika kikosi hicho. Bocco alisema kukosekana kwa wachezaji muhimu katika k… Read More
  • FARID MUSSA ASUBIRI RUHUSA YA AZAM FCFarid Mussa ni winga wa Azam FC aliyepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio katika klabu ya Deportivo Tenerife ya nchini Hispania na kufanikiwa kufuzu majaribio hayo na sasa anasubiri ruhusa ya klabu tu ili aondoke zake. … Read More
  • KIWANGO KIBOVU CHA HAJI MWINYI CHAMUUMIZA PLUIJMKiwango cha beki wa kushoto wa Yanga Haji Mwinyi kinaonekana kushuka hali inayomfanya kocha Hans Pluijm kutafuta namna ya kulifanyia kazi suala hilo. Haji Mwinyi ni beki mwenye kipaji kikubwa anayeweza kuimudu vizuri nafas… Read More

0 comments:

Post a Comment