Thursday, May 26, 2016

TAIFA STARS KUELEKEA NCHINI KENYA KESHO

Kikosi cha timu ya taifa ya mpira wa miguu Tanzania (Taifa Stars) kilichopo chini ya Charles Boniface Mkwasa kinatarajiwa kuondoka nchini kesho kuelekea Kenya kwa ajili ya mchezo wao wa kirafiki wa Kimataifa.


Stars itaondoka kesho majira ya saa 12 alfajiri kwenda Nairobi kenya, mchezo huo ni wa kujiandaa na Mchezo dhidi ya Misri utakaopigwa juni 4, 2016 katika kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON-2017).

0 comments:

Post a Comment