Thursday, May 26, 2016

SERENGETI BOYS KUTUA NCHINI LEO

Timu ya taifa ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (Serengeti Boys) inatarajiwa kuwasili nchini leo alhamisi Mei 26,2016 majira ya saa 1 na robo jioni ikitokea nchini India ilikoenda kushiriki mashindano maalumu ya Vijana yaliyoandaliwa na nchi hiyo na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa tatu.

TFF inawaalika waandishi wa habari na wadau wengine kuilaki timu ya soka ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ inayotarajiwa kutua leo Mei 26, 2016 saa 1.15 jioni baada ya kushika nafasi ya tatu katika michuano maalumu ya kimataifa iliyoandaliwa na Shirikisho la Soka nchini humo (AIF Youth Cup 2016 U-16).

Serengeti Boys haikuwahi kupoteza mchezo hata mmoja katika michuano hiyo baada ya kutoka sare mechi tatu na kushinda mmoja kabla ya kuingia hatua ya kucheza mshindi wa tatu ambako ilishinda mabao 3-0 jana dhidi ya Malaysia.

India kimeandaa mashindano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kikosi chao kwa ajili ya Fainali za Kombe la Dunia kwa Vijana zitakazofanyika nchini humo mwaka 2017.

Related Posts:

  • MATOKEO LIGI KUU BARA LEO SIMBA YATAKATA UHURU Simba imeendeleza wimbi lake la ushindi msimu huu baada ya  leo kuifunga timu ngumu ya kagera sugar ya mkoani kagera katika mchezo ulichezwa uwanja wa Uhuru jiji Dar es salaam, na hii inamainisha samba imeshinda mch… Read More
  • BAADA YA KUZUILIWA TAIFA, YANGA KUCHEZA HAPA Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea keshokutwa Jumatano Oktoba 12, 2016 kwa michezo saba huku ule mchezo kati ya Young Africans ya Dar es Salaam dhidi ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ukipangwa kufanyika… Read More
  • MATOKEO YA MICHEZO YA LEO VPL MATOKEO YA MICHEZO YA LEO VPL Uwanja wa uhuru tumeshuhudia mpira ukiwa ni wa kupaniana sana hasa kipindi cha kwanza ambapo kadi za njano nyingi zilitoka na huku kila timu ikionekana kutokumwamini mwamuzi Israel Nkongo. … Read More
  • RATIBA LIGI KUU BARA LEO JUMAPILI Michezo kadhaa kupigwa jumapili hii kote duniani tukianzia nyumbani Tanzania ligi kuu Tanzania Bara kuendelea katika viwanja vinne vya miji tofauti. Macho ya wapenda michezo wengi Afrika mashariki yapo uwanja wa Uhuru a… Read More
  • MO,MANJI KIKAANGONI OCTOBA 20,2016 CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimeandaa kongamano maalumu Oktoba 20 mwaka huu, kuzungumzia mifumo ya kiuendeshaji ambayo klabu kongwe nchini za Simba na Yanga zipo mbioni kuingia. Simba na Yan… Read More

0 comments:

Post a Comment