Friday, May 27, 2016

WACHEZAJI AZAM FC WAPEWA MAPUMZIKO

Wachezaji wa  Azam FC, wamepewa mapumziko ya wiki tano baada ya kumaliza mechi ya mwisho ya msimu wa 2015/16 dhidi ya Yanga kwenye mchezo wa fainali ya Kombe la Shirikisho (Azam Sports Federation Cup) juzi jioni.


Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, amesema kuwa msimu ndio umeisha kwa timu hiyo na kilichobakia ni kujipanga kwa ajili ya kupata matokeo mazuri msimu ujao.

“Tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumecheza mchezo wa fainali, ingawa matokeo yalikuwa si mazuri haikuwa malengo yetu, tulipanga kushinda lakini lazima tukubali ni matokeo ya mpira,” alisema.

Kawemba alisema wachezaji watamaliza likizo hiyo Juni 30 mwaka huu na Julai Mosi wataanza maandalizi ya msimu mpya.

“Kwa hiyo tutafanya nini kwa msimu ujao, tutamuongeza nani, tutamtoa nani hayo tutazungumza baadaye lakini sasa hivi tunawaomba washabiki wetu wawe watulivu na tutaendelea kujipanga,” alisema.

Azam FC ilikubali kichapo cha goli 3 - 1 katika mchezo wa fainali kombe la shirikisho dhidi ya Yanga, Hata hivyo Azam FC itaiwakilisha Tanzania mwakani katika kombe la shirikisho barani Afrika CAF

0 comments:

Post a Comment