Sunday, June 19, 2016

BOCCO ATAJA KILICHOWAPONZA AZAM FC

Nahodha wa timu ya Azam FC, John Bocco amesema kuwa kushindwa kupata mafanikio katika msimu uliopita kumechangiwa na kuwakosa wachezaji wao muhimu katika kikosi hicho.

Bocco alisema kukosekana kwa wachezaji muhimu katika kikosi kama vile, Farid Mussa, Paschal Wawa, Kipre Tchetche, Shomari Kapombe kuliwafanya wapoteze malengo yao yote na kwamba hilo pia limechangia kwa kiasi fulani kuondoka kwa kocha wao Stewart Hall.

"Ilituumiza sana kwa sababu malengo yetu ilikuwa ni ubingwa na kufika hatua ya makundi ya kombe la shirikisho Afrika, lakini ikawa tofauti" alisema Bocco.

Bocco ni miongoni mwa wachezaji wakongwe katika klabu ya Azam FC, katika msimu uliopita ameifungia timu yake jumla ya magoli sita. Bocco anaimani kuwa makocha wapya walikoja katika kikosi chao na usajili ukienda vizuri basi watafanya vizuri katika michuano mbalimbali ijao.

Like Ukurasa Wa Soka24 Facebook Hapa

Related Posts:

  • MBEYA CITY, YANGA KUSIMAMISHA JIJI LEO Ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom inatarajiwa kuendelea tena leo kwa mchezo  utakaowakutanisha Mbeya City ya Jijini Mbeya dhidi ya Yanga ya  jijini Dar-Es-Salaam. Yanga inaingia katika mchezo huu … Read More
  • AZAM FC YAICHAPA AFRICAN SPORTS Klabu Bingwa Afrika Mashariki na kati Azam FC ilikuwa ugenini jijini Tanga kupambana na African Sports katika mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara maarufu kama Vodacom. Azam FC wamefanikiwa kuibuka na ushindi katika mchezo h… Read More
  • NDANDA FC WAPANIA KUHARIBU SHEREHE YA YANGA Msemaji wa klabu ya Ndanda FC Idrisa Bandari amesema watahakikisha wanaifunga Yanga na kuharibu Sherehe yao ya kukabidhiwa kombe leo katika mchezo utakaopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar. Yanga wanaingia katika mc… Read More
  • SIMBA SC WAIDUNGUA MTIBWA SUGAR NYUMBANI KWAO SIMBA ilishuka dimbani hivi leo kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo wao wa 29 wa ligi kuu Tanzania bara,Mchezo uliopigwa mjini Morogoro. Mchezo huo umemalizika kwa Simba SC kushinda kwa goli 1 - 0 goli lililofungwa na… Read More
  • VITA YA KUWANIA NAFASI YA PILI VPL KUENDELEA TENA LEO LIGI kuu Tanzania bara inatarajia kuendelea tena leo katika viwanja viwili. Mjini Morogoro wakata miwa wa Mtibwa watawakaribisha vijana wa Msimbazi Simba SC wakati huko Tanga Azam FC itachuana na African Sports. Simba w… Read More

0 comments:

Post a Comment